Kwa Mafundi, Wamiliki wa Makampuni na Wawekezaji katika Sekta ya Ujenzi. Mafunzo haya ni katika kutengeneza mchanganuo wa gharama za ujenzi (B.O.Q), kukadiria vifaa vya ujenzi kutoka kwenye vipimio vya ujenzi wa nyumba, kutengeneza bei za kujaza kwenye mikataba wakati wa ujenzi, kujua makadirio ya kisoko ya gharama za ufundi kwa kila kazi na mwisho kujipatia bei ya vifaa vya ujenzi kutoka madukani. Mafunzo haya yote yanatumia mfumo wa kigitaili unaoitwa HALA BuildCostManage Software. unaopatikana kwa lugha zote mbili Kiswahili na kingereza , pia ambao umebuniwa kwa kutumia mazingira halisi ya Kitanzania.
Kwa Mafundi, Wamiliki wa Makampuni na Wawekezaji katika Sekta ya Ujenzi. Katika (Ujumla wa ubora wa kazi; Ukadiriaji wa gharama za ujenzi na namna ya kusoma ramani ya nyumba; Uaminifu katika kazi kama msingi wa kufikia thamani halisi ya mradi; Utaratibu wa kusajili mradi na kupata kibali cha ujenzi kutoka katika mamlaka husika)
Katika (Kujenga Kuta na Kusakafia, Kupaka Rangi Kwenye Kuta na dali, Kufunga Nondo Wakati wa Ujenzi, Kutengeneza Majukwaa na Kupaua na Kuweka Malumalu Kwenye Sakafu)
Mafunzo ya sheria za ujenzi Kwa Mafundi, Wamiliki wa Makampuni na Wawekezaji katika Sekta ya Ujenzi. Mafunzo juu ya sheria za ujenzi katika maeneo yaliyopimwa (Surveyed area) na maeneo ambayo hayajapimwa (un-surveyed area), mahitaji yanayohitajika wakati wa ujenzi wa nyumba isiyo gorofa na nyumba ambayo ni gorofa na sheria zinazotumika katika sekta ya ujenzi, pamoja na mamlaka zinazohusika wakati waujenzi.